" KIWANDA CHA L&N PACKING SOLUTION CHAOMBA MASOKO NA MSAADA WA SERA, CHALENGA KUONGEZA UZALISHAJI NA AJIRA.

KIWANDA CHA L&N PACKING SOLUTION CHAOMBA MASOKO NA MSAADA WA SERA, CHALENGA KUONGEZA UZALISHAJI NA AJIRA.


Fabius Clavery -Misalaba Media-Kagera.

‎Kiwanda cha kuzalisha na kusindika vifungashio (Magunia) cha L&N packaging solutions kilichopo wilayani Missenyi mkoani Kagera kimewaomba  wadau wa sekta ya umma na binafsi kuongeza uagizaji wa bidhaa zake, kikisema kina uwezo mkubwa wa uzalishaji lakini bado kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa masoko ya uhakika.

‎Bi,Batreth Jacob Rwiguza,Mkurugenzi wa kiwanda hicho,ameeleza kuwa mitambo iliyopo kiwandani hapo ina uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kikubwa ambapo inazalisha vifungashio tani 3 kwa saa 16 na kwa ubora unaokidhi viwango, licha yakuwa kwa sasa kiwanda hicho bado kinakabiliwa na changamoto ya masoko yakutosha.

‎"Kwa sasa tunazalisha kwa Oda,Tunashukuru wadau wanatuoa oda  tunazalisha licha ya kwamba madoko hayajawa makubwa sana, lKini kiwanda chetu kina uwezo mkubwa wa kuzalisha, tuna wafanyakazi na miundombinu ya kutosha, Changamoto kwa sasa ni masoko na gharama za uendeshaji kutokana na kwamba uagizaji wa malighafi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji  gharama kodi ni kubwa,” amesema .zake

‎Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo ameiomba Serikali kuangalia upya viwango vya kodi na tozo kwenye uingizaji wa malighafi kutoka nchi wazalishaji, akisema kuwa kupunguza kodi hizo kutakiwezesha kuingiza malighafi bora kwa gharama nafuu, hali itakayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ushindani wa bidhaa zake sokoni.

‎Kadhalika Bi Batreth ameiomba serikali kuangalia namna ya kuimarisha Upatikanaji wa nisahati ya Umeme kwani kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika eneo hilo kunasababisha hasara

‎"Tunaiomba serikali itusaidiw katika eneo la Umeme kwa sababu umeme ukikatika kwa mfano malighafi zinazokua zinachakatwa muda huo umeme ukikatika zinaharibika huwezi kuzitumia tena" ameongeza Mkurugenzi huyo

‎Kupatikana kwa masoko ya uhakika pamoja na mazingira rafiki ya kodi, utaongeza uzalishaji, kuimarisha uendeshaji wa kiwanda na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

‎Mbali na uzalishaji, kiwanda Cha  L&N PACKING SOLUTION ni  chanzo muhimu cha ajira kwa wananchi wa eneo la Missenyi, ambapo kinawaajiri wafanyakazi wa kudumu na wa muda.

‎Aidha, uwepo wa kiwanda hicho umefungua fursa nyingine za kiuchumi ikiwemo biashara ndogondogo, huduma za usafirishaji wa malighafi na bidhaa, pamoja na shughuli za kibiashara kwa jamii inayokizunguka.





  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post