" MIKAKATI LUKUKI YAWEKWA BARAZA LA MADIWANI JIJI LA ARUSHA

MIKAKATI LUKUKI YAWEKWA BARAZA LA MADIWANI JIJI LA ARUSHA

Na, Egidia Vedastio,

Misalaba Media, Arusha.

Katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka,Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe ametia uamsho wa kuweka mikakati katika maandalizi ya kuelekea  AFCON 2027.


Amesema kuwa katika nchi jirani za Afrika mashariki mabango ya kukaribisha mashindano hayo yameshaanza kuwekwa tofauti na ilivyo katika nchi yetu hususan Jiji la Arusha ambapo ndio mwenyeji wa ugeni huo.


Aidha Iranqhe amelitaarifu baraza hilo kuwa wamejipanga kujiendesha kwa mapato ya ndani bila kutegemea ruzuku kutoka serikali kuu. 

Amesema uchumi wa halmashauri ya Jiji unaweza kufanikisha hilo kwa kuiga nchi ya china ambayo imefanikiwa  kwa kuwekeza katika serikali za mitaa.

"Huu ni wakati muafaka wa kuboresha eneo la stendi ndogo, eneo hilo litaboreshwa bila kuwabugudhi wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo, sambamba na hayo uwekezaji katika masoko yetu unatakiwa kufanyika, hii yote ni kutafuta kupandisha hadhi ya Jiji, kuangalia uwekezajibwa kiwanda cha nyama Arusha Meat, mikopo kwa watu wenye ulemavu, wananwake na vijana.Hatua hizi zikikamilika mapato ya serikali yataongezeka" amesema Iranqhe.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Joseph Mkude amewataka Madiwani kudumisha ushirikiano, uwajibikaji, nidhamu, kufuata misingi ya kazi na kuwasikiliza wananchi badala ya kuwavunja moyo.

Vilevile ametoa rai kwa watendaji wanaowakwamisha wanaoomba mikopo ya halmashauri. Amesema kuwa pesa zimekuwa zikibaki katika mfuko wa maendeleo ya jamii kitu ambacho ni kukiuka utaratibu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.


Kuna mambo mbalimbali yanatakiwa kuangaliwa upya ikiwemo kukithiri kwa adhabu mashuleni, hamasa ya kujiunga na bima ya afya kwa wote, wazazi kutotozwa michango, matumizi ya rushwa na mengine mengi",

"Kipindi hiki kila mmoja ni shahidi wa mabadiliko ya tabia ya nchi, wahimizeni wananchi kutunza chakula" amesema Mkude.

Katika namna hiyohiyo Diwani wa kata ya UngaLimited Mahmoud Said akichangia hoja yake, ameomba kuwekwa matuta katika barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km1.8 ili kuepushia wananfunzi ajali.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post