" SERIKALI NA BARAZA LA DHAHABU DUNIANI KUONGEZA THAMANI SEKTA YA DHAHABU

SERIKALI NA BARAZA LA DHAHABU DUNIANI KUONGEZA THAMANI SEKTA YA DHAHABU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dhahabu Duniani (WGC), Bw. David Tait, pamoja na Waheshimiwa Mawaziri baada ya mazungumzo ya kimkakati.
Majadiliano hayo yamelenga kuboresha mnyororo wa thamani wa sekta ya dhahabu nchini, hususani katika kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo ili kukuza mchango wao katika uchumi wa taifa.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Katika kutekeleza sera ya kutosafirisha madini bila kuongeza thamani, serikali imekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dhahabu Duniani (World Gold Concil) Bw. David Tait juu ya kuendeleza sekta ya dhahabu nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Februari 13, 2026 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) ameongoza Mawaziri wanne, Mawaziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima katika mazungumzo hayo.

Mazungumzo hayo yameangazia namna ya kuirasimisha sekta ya wachimbaji wa dhahabu wadogo ili kuhakikisha wanafanya uchimbaji wenye faida bila kuathiri mazingira.

Aidha, wamejadili namna ambavyo baraza hilo litashiriki kuiwezesha Tanzania kuvutia wawekezaji zaidi katika kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa nchini ikiwa ni utekelezaji wa sera na sheria za sasa ambazo haziruhusu kuuza na kusafirisha madini bila kuongeza thamani.

Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Baraza la madini duniani limevutiwa na namana serikali invyojenga mfumo mzuri wa kuwawezesha wachimbaji wadogo ambao huchangia uzalishaji wa madini kwa asilimia 40, huvyo kulifanya baraza hilo kuiona Tanzania ikiwa ni sehemu salama ya kufanya ushirikiano katika kukuza sekta hiyo.

Kwa upande wake Bw. Tait Amesema kuwa Baraza la Dhahabu duniani linavutiwa na namna serikali ya Tanzania inavyowawezesha wachimbaji wadogo, na hivyo ushirikia baina ya shirika hilo utakuwa ni kitovu na kielelezo cha namna sekta ya inavyoweza kukua na kuongeza tija.



Post a Comment

Previous Post Next Post