Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameshiriki katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wazee wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Barani Afrika (AWLN Elders High-Level Meeting), uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Afrika tarehe 13 Februari 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wanawake mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika kwa lengo la kuimarisha malezi, ushauri na uongozi wa kizazi hadi kizazi.Aidha, washiriki walijadili kwa kina utekelezaji wa kimkakati wa Ajenda 2063, wakisisitiza umuhimu wa maendeleo jumuishi na endelevu yatakayowanufaisha wananchi wote wa Afrika.Kupitia ushiriki huo, Tanzania imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuendeleza usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake katika nafasi za maamuzi, na kuchangia kikamilifu katika ajenda za maendeleo ya bara la Afrika.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii TanzaniaMhe. Maryprisca Mahundi (Kushoto) akiwa na Rais wa Kwanza MwanamkeBarani Africa Kutoka Liberia Bi. Elen Johnson Sirleafwakiwa Ethiopia 13/02/2026🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment