Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Mhimiri wa mahakama umekumbushwa kutenda haki kwa wananchi bila ubaguzi kama miiko na taratibu za kazi zinavyowataka.
Akizungumza katika kilele cha siku ya sheria nchini katika viwanja vya mahakama kuu Arusha Hakimu mfawidhi wa mahakama kuu Kanda ya Arusha Jaji Frank Mahimbali amesisitiza watendaji wake kuepuka vitendo vya rushwa na kujiamini katika utendaji wao.
Aidha ameeleza kuwa katika mwaka wa mahakama ulioisha wamefanikiwa kumaliza mashauri kwa asilimia kubwa na kufikia malengo yao kama ilivyotakiwa.
"Vitendo vya kejeli juu ya mahakama havitavumilika, kwa sababu tunafanya kazi zetu kwa kufuata kanuni na taratibu zetu, tukifuata miiko na taratibu zilizowekwa. Kwa msingi huo tutahakikisha tunasimamia uadilifu na kuwasha taa mahali penye giza",
"Katika malengo yetu ya msingi ni kuhakikisha kesi zinasikilizwa na kukamilika ndani ya muda, ambapo mahakama ya mwanzo inakamilisha mashauri yake kwa miezi mitatu, mahakama ya wilaya miezi sita na mahakama kuu kwa mwaka mmoja. Tunajivunia sana hatua hiyo na tutaendelea kutumia mfumo wa TEHAMA na kuwajengea uelewa wananchi juu ya matumizi hayo" amesema Jaji Mahimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Mahakama kusikiliza na kukamilisha mashauri kwa wakati.
Hata hivyo amewakumbusha kutenda haki, kuepuka vitendo vya rushwa, kuepuka ubaguzi wa rangi, wenye kipato na wasio na kipato.
"Serikali itaendelea kuwaonyesha ushirikiano wa kina, mkafanye kazi kwa uaminifu na haki na kutoa elimu kwa wananchi ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima kwenda mahakamani na kutatuliwa na utawala.
Katika namna hiyohiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Chapter ya Arusha Wakili Hamis Mkindi amesema serikali inatakiwa kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi ili kuepuka migogoro na machafuko yasiyokuwa ya lazima.
Hata hivyo amebainisha kuwa ustawi wa maendeleo ya Taifa unategemea mihimili mitatu ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge, na mihimili hiyo inatakiwa kuwasikiliza wananchi ili kulinda amani, utulivu na uchumi wa wananchi.
" Ni dhahiri kuwa mageuzi ya kimuundo yameleta mafanikio katika mnyororo wa haki, tutaendelea kushirikiana Mawakili wa kujitegemea na wa serikali lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa kisheria" amefafanua Jaji Mkindi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment