Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Segese, iliyopo Kata ya Segese katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, ulinzi shirikishi na umuhimu wa utii wa sheria bila shuruti.Akizungumza na wanafunzi hao, Mkaguzi wa Polisi Adela Kimaro, ambaye ni Polisi Kata ya Segese, alieleza kuwa ukatili wa kijinsia ni kosa la jinai linalokiuka haki za binadamu na linaathiri maendeleo ya jamii, hususan kwa vijana na wanafunzi. Aliwataka wanafunzi kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili, kutoa taarifa mapema wanaposhuhudia au kufanyiwa vitendo hivyo, na kujenga utamaduni wa kuheshimiana shuleni na katika jamii.Pia alisisitiza kuwa ulinzi shirikishi hujenga mshikamano na kuzuia uhalifu kabla haujatokea hivyo ni wajibu wa kila mwanafunzi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu kabla havijatokea.Aidha, kuhusu utii wa sheria bila shuruti, Mkaguzi Kimaro aliwahimiza wanafunzi kujenga nidhamu binafsi na kufuata sheria na kanuni kwa hiari, bila kulazimishwa, ili kujenga jamii yenye maadili, amani na utulivu.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment