" PPAA YAFUNGUA FURSA KWA VIJANA 878, YAZUIA ZABUNI ZA TZS BILIONI 586

PPAA YAFUNGUA FURSA KWA VIJANA 878, YAZUIA ZABUNI ZA TZS BILIONI 586






‎Na. Meleka Kulwa

‎Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani za Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando, amesema kuwa Mamlaka imefungua fursa kwa vijana 878 kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kudai haki zao kwa ufanisi katika michakato ya ununuzi wa umma.

‎Ameyabainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana leo Februari 25, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mtumba jijini Dodoma.

‎Amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuwawezesha vijana na makundi maalum kushiriki kikamilifu katika sekta ya ununuzi wa umma.

‎Aidha amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Mamlaka imeendelea kutekeleza jukumu lake la kusimamia na kushughulikia rufaa zote zinazotokana na michakato ya ununuzi wa umma kwa misingi ya haki, uwazi na uadilifu.

‎Pia ameongeza kuwa katika baadhi ya mashauri yaliyosajiliwa, Mamlaka imezuia utoaji wa tuzo za zabuni 43 zenye thamani ya TZS 586,502,801,992/= kwa wazabuni waliokosa uwezo wa kifedha na sifa za kitaalamu za kutekeleza zabuni husika.

‎Amesema kuwa hatua hiyo imezuia utekelezaji usioridhisha wa miradi ambao ungesababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.

‎Aidha amebainisha kuwa Mamlaka imeendelea kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) kupitia Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Malalamiko na Rufaa, hatua iliyoongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika mchakato mzima wa ununuzi wa umma.

‎Pia ameongeza kuwa Mamlaka itaendelea kushirikiana na mamlaka nyingine kuboresha mifumo ya utoaji wa haki katika michakato ya ununuzi wa umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, stahiki na kwa wakati.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post