Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kufanya urasimishaji wa namba za usajili za vyombo hivyo pasipo shuruti mara baada ya kibali Cha muda mfupi kuisha.Akitoa elimu hiyo Kwa madereva wa vyombo vya moto Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa kuendesha vyombo vya moto Kwa kutumia namba ya chasi (chasiss number) bila namba ya usajili ni kosa kisheria mara baada ya muda wa kibali hicho Cha muda mfupi kuisha.Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kujisimamia na kutekeleza takwa la kisheria bila shuruti pindi wanapotoa vyombo hivyo bandarini au kuvinunua vikiwa na namba ya chasi (chassis number)
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment