
Kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam , Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imethibitisha kuwa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika 2027 haitaahirishwa, licha ya kuwepo kwa wasiwasi kuhusiana na maandalizi ya Miundombinu na hali ya hewa ya kisiasa katika nchi waandaaji.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Juni-Julai 2027, licha ya wito kutoka kwa Mwenyeji mwenza Kenya kufikiria kuahirishwa kutokana na hatari ya vurugu zinazohusishwa na Uchaguzi uliopangwa kufanyika kwa muda huo huo.
CAF imesalia kuwa na msimamo imara, huku timu ya ukaguzi ikiendelea na kazi yake katika nchi tatu za Tanzania,Kenya na Uganda.
CAF imesisitiza dhamira yake ya kuimarisha Waamuzi na Nidhamu, maeneo mawili yaliyochukuliwa kuwa muhimu ili kuhakikisha uaminifu wa mashindano ya Afrika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment