Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaBodi ya Nishati Vijijini (REB) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kusambaza gesi asilia katika eneo la Kisemvule, wilayani Mkuranga mkoani Pwani, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 6.8 zimewekezwa kuwezesha wananchi kupata nishati safi na salama ya kupikia.Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania na kufadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi.Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Jacob Kingu, amesema utekelezaji wake unaonesha dhamira ya Serikali kuboresha maisha ya wananchi na kulinda mazingira kwa kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.“Huu ni mradi wa kimkakati unaotekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuona Watanzania wengi wanatumia nishati safi. Tunapaswa kulinda miundombinu hii kwa kuwa imegharimu fedha nyingi za Serikali,” amesema.Kwa mujibu wa REA, mradi huo ulilenga kuhudumia kaya 2,000, huku hadi sasa kaya 530 zikiwa zimeunganishwa katika eneo lenye wakazi zaidi ya 64,000, hatua inayofungua fursa ya kupanua zaidi huduma hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa REA, Hassan Saidy, amesema taasisi hiyo imeiomba TPDC kufanya tathmini katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambako bomba la gesi limepita, ili kuanzisha miradi ya ubia itakayowezesha wananchi wengi zaidi kuunganishwa.Wananchi wa Kisemvule wameeleza kunufaika na mradi huo kwa kupungua gharama za nishati na urahisi wa upatikanaji wa gesi asilia, huku mradi ukiendelea kuwa mfano wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nishati Safi nchini.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment