
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataka Madereva wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.
Amezungumza hayo wakati akifungua Mafunzo ya siku moja kwa Madereva wa Jeshi la Polisi mkoani humo yaliyofanyika katika ukumbi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mbeya Februari 18, 2026.
Kamanda Kuzaga ameeleza lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na weledi Madereva katika uendeshaji wa Magari ya Polisi na Serikali kwa kuzingatia sheria zote za usalama barabarani na kuepuka kuwa chanzo cha ajali kwa Madereva wengine.
Aidha, Kamanda Kuzaga amesisitiza na kuwataka Madereva hao kutunza mali za Serikali (Magari) kwa kuhakikisha wanafuata sheria na miongozo ya Jeshi la Polisi katika suala la utunzaji na uendeshaji wa vyombo vya moto vya Serikali ikiwemo Jeshi la Polisi.
Naye, Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Notker Kilewa ameeleza kuwa wamejiandaa kuwajengea uelewa na uwezo Madereva hao katika kutambua Sifa za Madereva wa Serikali, Ukaguzi wa Magari, Makosa hatarishi, vyanzo vya ajali na suala la msongo wa mawazo.
Aliongeza kuwa, ni matarajio kuwa Mafunzo hayo yatasaidia kuwakumbusha na kuwajenga Madereva kufahamu sheria, miongozo na taratibu nyingine wawapo barabarani na kuliwakilisha vizuri Jeshi la Polisi hasa kwa kuepuka kufanya makosa ambayo yanaweza kusababisha ajali na uharibifu wa mali za Serikali.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment