
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Brig. Jen. Ahmed Abbas Ahmed, amewataka wabunge wote wa mkoa huo kuweka tofauti zao pembeni na kushirikiana kwa pamoja katika masuala ya kimkoa, ili waweze kuzungumza kwa sauti moja ndani ya Bunge na kuhakikisha changamoto na mahitaji ya wananchi wa Ruvuma yanapatiwa ufumbuzi.Akizungumza wakati wa Baraza la Ushauri la Mkoa lililofanyika katika ukumbi wa Songea Club uliopo Manispaa ya Songea, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa licha ya kila mbunge kuwa na wajibu wa kushughulikia changamoto za majimbo yake, bado kuna masuala ya kimkakati yanayohusu mkoa mzima ambayo yanahitaji umoja na msimamo wa pamoja.Amebainisha kuwa umoja wa wabunge utasaidia kuongeza nguvu ya hoja wanapowasilisha masuala ya maendeleo bungeni, jambo litakalosaidia kuvutia rasilimali na miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote wa Ruvuma.Aidha, amewataka wabunge kuyachukua mambo yote yaliyojadiliwa katika baraza hilo na kuyabeba kwa uzito unaostahili, kisha kupaza sauti ili kusaidiwa Kwa upande wao wabunge wa mkoa wa mkoa wa Ruvuma wameonesha kuungana na kauli hiyo ya mkuu wa mkoa na kueleza nia yao ya dhati kwa pamoja kuhakikisha wanaweka mbele maslahi ya mkoa bila kujali tofauti zao za kijimbo na kiitikadi
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment