" VIJANA KUWENI CHACHU YA MAENDELEO

VIJANA KUWENI CHACHU YA MAENDELEO

Ndugu Idd Hassan Kimanta, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, mgeni rasmi katika maadhimisho ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mpanda, tarehe 02 Februari 2026.🔰VIJANA KUWENI CHACHU YA MAENDELEO Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wamefanya sherehe kuelekea Maadhimisho ya Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM leo Tarehe 2 February 2026Akizungumza na Vijana wa Wilaya ya Mpanda Mgeni Rasmi Ndugu Idd  Hassan Kimanta Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (MNEC) amewataka vijana Kuwa chachu ya Maendeleo kwa kuchangamkia Fursa mbalimbali ambazo zinapatikana Katika jamii inayowazunguka ikiwemo uthubutu wa kuwania nafasi mbalimbali za UongoziKatika hatua nyingine amewataka vijana kuendelea kuchagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa letu Kama isemavyo kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCMKatika hatua nyingine Ndugu.Idd Hassan Kimanta Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu  (MNEC) ameongoza kundi la vijana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda kupanda Miti zaidi ya 500 ya matunda na vivuli Katika eneo la Ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha Kata ya IbindiTumechagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa letuNdugu Kabalila, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mpanda akizungumza.Bi. Aziza Said Self, Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Mpanda.Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, tarehe 02 Februari 2026 ameshirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuadhimisha miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ibindi, Halmashauri ya Nsimbo.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post