
Afisa Kazi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Veronica Maro akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Mfumo wa Taifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira kwa washiriki kutoka Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri na Mashirika katika ukumbi wa NSSF leo Februari 23, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Na: OWM (KAM) – Dar es Salaam
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri na Mashirikisho nchini waaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia ili kuongeza tija, uwazi na ufanisi katika maeneo ya kazi.
Wito huo umetolewa wakati mafunzo ya Mfumo wa Taifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira yaliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira Mahusiano kwa Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri na Mashirikisho leo Februari 23, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Afisa Kazi Mkuu, Veronica Maro, amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuratibu, kukusanya, kuchambua na kuweza kutangaza taarifa za soko la ajira kwa wakati, hivyo amesisitiza matumizi mfumo huo yanaweza kurahisisha utoaji wa huduma kwa kupata wataalamu wanaohitaji ndani ya taasisi zao kupitia soko la ajira.
Vile vile, amesema kupitia mfumo watapata fursa ya kutangaza nafasi za kazi sambamba na kuwasiliana na wahitaji wa ajira wenye sifa stahiki kwa njia rahisi kupitia mfumo huo.
Kwa upande mwengine, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri itaendelea kuratibu, kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo huo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo.
Naye, Mwakilishi wa Chama cha Madereva Tanzania (TADU), Ramadhani Selemani ameipongeza serikali kwa mfumo huo na kueleza kuwa utasaidia kuingiza taarifa za soko la ajira na kuzifikia kwa wakati.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi ya Hotel, Huduma ya Jamii na Ushauri (CHODAWU), Asteria Gerald ameeleza utayari wao wa kuhamasisha matumizi ya kidijitali katika utoaji wa taarifa na huduma kwa wanachama, huku wakiahidi kuendeleza matumizi ya wa Taifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira katika kipindi hiki cha mageuzi ya teknolojia ili kukuza soko la ajira.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment