" JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA LAWADAKA WATU WATATU KWA UTAPELI

JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA LAWADAKA WATU WATATU KWA UTAPELI






Na Mwandishi Wetu,Ruvuma

JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma,linawashikilia watu watatu wa tuhuma za kutapeli Sh.milioni 147 kutoka kwa mfanyabiashara na wakala wa CRDB Paulo Akweso baada ya kumlaghai awapatiwe fedha hizo ili wazifanyie dawa na ziweze kuongezeka.

Kamnda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Marco Chillya alisema,tukio hilo limetokea tarehe 2 Februari mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya Mwandapoli iliyopo eneo la Bombambili Manispaa ya Songea.

Kamanda Chillya alieleza kuwa,baada ya wakala huyo kuambiwa hivyo alitoka katika nyumba hiyo ya kulala wageni ambayo alikuwa amepangisha na kwenda kwa mawakala wadogo tisa na kukusanya fedha na kuwaambia anakwenda kuwawekea katika akaunti zao za benki ili waendelee kutoa huduma kwa wateja.

“Lakini wakala huyo hakwenda benki kama alivyowaambia mawakala hao wadaogo badala yake alikwenda nazo katika nyumba ya kulala wageni ama alivyoelekezwa na matapeli ambao walimwambia azitandaze fedha kitandani kasha azipake na aondoke katika chumba hicho bila kufunga mlango ili malaka waweze kuzichukua na watazirudisha zikiwa zimeongezeka”alisema Chillya.

Alisema,wakala aliondoka na baada ya saa moja alirudi chumbani na kukuta fedha zote hazipo kwa kuamini kwamba malaika wamezichukua na kukaa chumbani kwa muda mrefu akisubiri zirudi,hata hivyo hazikurudi mpaka bosi wake Thadei Kimaro alipopata taarifa na kwenda kituo cha Polisi Songea kutoa taarifa.

Chillya alisema,baada ya Polisi kupata taarifa walifuatilia tukio hilo na tarehe 17 Februari 2026 Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili Enosta Kangapi(maarufu bosi hanuniwi miaka 36) na Kelvin Kangapi(37).

Alisema,watuhumiwa hao wamekamatwa katika mtaa wa Uhindini Mkoani Dodoma na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika kufanya tukio hilo wakishirikiana na mwenzao Salva Komba(chura)ambaye alikamatwa tarehe 18 maeneo ya stendi kuu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa Kamanda Chillya,baada ya upelelezi Enosta Kangapi( bosi hanuniwi)ambaye ni kiongozi wa kundi hilo katika akauti yake zilikutwa Sh.milioni 88 ambazo alikiri kuwa sehemu ya fedha walizotapeli na fedha nyingine akiwa amenunua pikipiki 4 na viwanja vitatu huko wilayani Mbinga.

Pia alisema,wamewakamata wahalifu wa matukio ya uvunjaji na vibaka(vishandu)wanaojihusisha kupora mikoba ya akina mama nyakati za usiku ambapo katika operesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata wahalifu 22 kati yao mwanamke mmoja na pikipiki 38 zisizokuwa na namba za usajili.

“Pikipiki hizi zilikuwa zikitumika katika uporaji maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea,na tumefanikiwa kukamata televisheni 9,Radio aina ya Subwoofer 8 na pombe ya moshi(gongo)lita 53 ambapo Televisheni 4 na Radio 2 zimetambuliwa na kukabidhiwa kwa wahusika”alisisitiza Kamanda Chillya.

Ametoa onyo kali na kuwakumbusha wahalifu wote kuwa,Mkoa wa Ruvuma sio sehemu ya salama kwao ya kufanya vitendo vya uhalifu badala yake watafute shughuli halali zitakazowaingizia kipato.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post