Na Fabius Clavery Misalaba Media-Kagera.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kuvunja mipaka katika sekta ya elimu kwa kuwawezesha waalimu wenye ulemavu wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwapatia vifaa vya kufundishia vya kidigitali na teknolojia saidizi ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha elimu jumuishi, kuhakikisha usawa na kutambua mchango wa waalimu wote bila kujali hali zao za kimwili kwenye kuleta mapinduzi ya Elimu nchini.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Waalimu wenye ulemavu watano (5) kutoka kwenye shule za Sekondari na Msingi wilayani humo, Mapema tarehe 10/02/2026 na Afisa Elimu Sekondari Ndg. Wandere Lwakatare kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karagwe katika Ofisi za idara ya Elimu Sekondari.
Aidha, Ndg. Lwakatare amesema kuwa vilivyokabidhiwa ni kompyuta mpakato, kishikwambi, vifaa maalum vya usomaji na uandishi (Perking Breiler) kwa walimu wenye uoni hafifu, Vinasa sauti , kofia na mafuta kwa waalimu wenye ulemavu wa ngozi.
“ Namshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia mradi wa Global Partnership for Education - Teachers Support Programme (GPE - TSP) kwa kuwapatia vifaa hivi Waalimu wetu wenye uhitaji maalumu kwasababu vitakua nguzo muhimu kwa waalimu na ninaamini vitaongeza ufaulu na utendaji wao utakua mahiri na wenye manufaa zaidi” Alisema Ndg. Lwakatare.
Akizungumza kwa niaba ya waalimu hao, Mwl. Basil Kashabano ambaye pia ni Katibu wa chama cha wasioona Tanzania Tawi la Karagwe amesema kuwa, Wamefurahi kupata vifaa hivyo na wanaishukuru Serikali kwa kuwafungulia milango ya kutumia teknolojia kama walimu wengine itakayo wawezesha kushiriki kikamilifu katika kujenga elimu bora. Pia, wamejisikia kuthaminiwa, kutambuliwa na wameahidi kufanya kazi kwa bidii.
Idara ya Elimu Msingi na Sekondari ina jumla ya waalimu 14 wenye mahitaji maalum kati yao waalimu 5 wamepatiwa vifaa hivyo kwa awamu ya kwanza na wengine wanatarajia kupatiwa kwa awamu zijazo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









Post a Comment