" NAIBU WAZIRI HAMIS MWINJUMA (MWANA FA) KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI

NAIBU WAZIRI HAMIS MWINJUMA (MWANA FA) KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI






Na Mapuli Kitina Misalaba
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, ni mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), unaofanyika katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma, Februari 12 na 13, 2026.


Mkutano huo unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utangazaji wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari, watangazaji, wahariri, wataalamu wa mawasiliano pamoja na washirika wa maendeleo, kwa lengo la kujadili mustakabali wa sekta hiyo nchini.


Kaulimbiu ya mkutano huo ni, “Matumizi ya Teknolojia katika Kupanua na Kuboresha Huduma za Utangazaji Vijijini,” ikilenga kuangazia namna teknolojia inavyoweza kusaidia kufikisha huduma za utangazaji katika maeneo ya vijijini na pembezoni ambako upatikanaji wa taarifa bado ni changamoto.


Katika mkutano huo, matukio mbalimbali yanaendelea ikiwemo mawasilisho ya mada, mijadala ya wazi, pamoja na maonyesho ya teknolojia mpya zinazoweza kutumika katika kuboresha utangazaji.


Washiriki wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidijitali.


Mkutano huo unatarajiwa kuibua mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha huduma za utangazaji, hususan katika maeneo ya vijijini, na kuongeza ubora wa maudhui kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia ya kisasa.













































































  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post