Na Fabius Clavery Misalaba Media-Kagera.
Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe limejadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo, yenye jumla ya shilingi bilioni 69.5 kwaajili ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo 10/02/2026 katika ukumbi wa Halmashauri (Angaza),Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe , Bi. Happiness J. Msanga amesisitiza umuhimu wa kila Mfanyakazi kutimiza wajibu wake kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha utekelezaji wa mipango na malengo yaliyokusudiwa na Taasisi.
“ Niwaombe tuliopo hapa tutumie nafasi hii ya uwakilishi kuwasihi wenzetu kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa kwasababu hakuna haki bila wajibu. Tuboreshe uwajibikaji na tuwe mabalozi wazuri wa kuelimishana namna ya kuomba madai na stahiki zetu kwa kufuata sheria badala ya kufoji taarifa pia Niwapongeze watumishi wanaotekeleza majukumu yao vizuri na kuifanya Halmashauri yetu iendelee vizuri” Alisema Bi.Msanga.
Aidha, Bi. Msanga amesema kuwa Bajeti hiyo imelenga, Uendelezaji ujenzi wa miradi yenye muelekeo wa kuiongezea Halmashauri Mapato, Ujenzi wa Maabara katika Shule za Sekondari za Kata, Upimaji na ulipaji fidia wa maeneo yote ya Taasisi za Halmashauri, Uendelezaji uzalishaji miche ya Kahawa, Ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Nyakakika, Uendelezaji ujenzi wa Matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari .
Badhi ya wajumbe wameomba bajeti hiyo kuwatazama pia wafanyakazi hodari,hasa wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ili kuendelea kuwapa morali wakati wa Utekelezaji wa Majukumu yao,Hoja hiyo imejibiwa kuwa kiasi za shillingi Laki 500,000 zimetengwa kwa ajaili hiyo kwa kwa kila idara .
Baraza la Wafanyakazi limehuduriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Wakuu na wawakilishi wa watumishi kutoka idara na vitengo , Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi TALGWU, TUGHE, CWT na CHAKUWAWATA kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment