" AIRTEL YAFUNGUA MADUKA MAPYA MANNE ARUSHA

AIRTEL YAFUNGUA MADUKA MAPYA MANNE ARUSHA

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania yapanua wigo wa kibiashara kwa kufungua maduka manne kwa mkupuo Jijini Arusha. 

Akifungua duka la Airtel Tripple A Jijini Arusha Katibu Tarafa, tarafa ya Elerai Chausiku Baha akimwakilisha Mkuu wa wilaya Arusha Mjini Joseph Mkude amesema kufunguliwa kwa maduka mapya ya airtel ni mwanzo wa fulsa lukuki kwa vijana kujipatia ajira na taifa kukuza pato lake.


Aidha ametoa ufafanuzi kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA takribani laini za simu 106 zimesajiriwa, hatua hiyo ikionyesha ukuaji na kukubalika kwa huduma za simu za airtel.

"Mawasiliano yanafungua fursa za uwekezaji na kukuza biashara.kwa ishara hii, mimi ni miongoni mwa watumiaji wa mtandao wa airtel na ninajivunia huduma zao nzuri kila wakati, naamini upanuzi wa huduma hizi utaleta tija katika sekta ya mawasiliano" amesema Chausiku.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kanda ya kaskazini Adriana Lyamba amesema huduma nyingi zinatolewa kidigitali, wateja wanahudumiwa haraka na kwa ufanisi.


"Siku ya leo tumezindua maduka manne hapa Tripple A, Ngaramtoni, Morombo na chuo cha uhasibu Arusha IAA, hii ni fursa kwa vijana wa Arusha kuchangamkia fulsa za ajira. Mkoa wetu ni lango la utalii hivyo huduma za mawasiliano ni mhimu ziongezwe ili wageni wanapoingia kwetu wafurahie huduma za mawasiliano" amesema Adriana.

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa simu wa kampuni ya airtel Thomas Mollel amesema ametumia mtandao huo kwa zaidi ya miaka kumi na tano, una ofa nyingi, na huduma zao ni nzuri.

" Nimefurahia kusogeza huduma zao karibu, natajia kumiliki aimu janja hivi karibu, hivyo ntafaidika na vifurushi vya intaneti"amesema Thomas.


  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post