" KANALI KIDO AFIKA OFISI ZA CCM KAGERA, AHAIDI USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANANCHI

KANALI KIDO AFIKA OFISI ZA CCM KAGERA, AHAIDI USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANANCHI

Na Fabius Clavery Misalaba Media-Kagera.

‎Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, amefika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera kwa lengo la kusalimia na kujitambulisha kwa viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na Wilaya, Februari 12, 2026, ikiwa ni siku moja tu tangu awasili mkoani humo.

‎Kanali Kido ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Stephen Ndaki, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mweshimiwa. Erasto Sima.

Mkuu huyo wamkoa amepokelewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mkoa wa Kagera, Ndg. Kareem Amri (MNEC), kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na viongozi wengine wa chama.

‎Akizungumza katika salamu zake za utambulisho, Kanali Kido amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Amesisitiza kuwa yupo tayari kushirikiana kwa dhati na viongozi wa chama pamoja na watendaji wa serikali ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya serikali unalenga kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

‎Kwa upande wake, MNEC Kareem Amri amempongeza Kanali Kido kwa uteuzi huo, akieleza imani ya chama kuwa atatekeleza majukumu yake kwa weledi na uadilifu. Aidha, amemkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM akimtaka kuitumia kama mwongozo katika kusimamia na kutekeleza ahadi zilizotolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.

‎Ziara hiyo ya utambulisho imeashiria mwanzo wa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Kagera unaimarika zaidi.




 
  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post