" WAZIRI KIKWETE: DUMISHENI UPENDO, UAMINIFU NA USHIRIKIANO KWA MSINGI WA MAENDELEO

WAZIRI KIKWETE: DUMISHENI UPENDO, UAMINIFU NA USHIRIKIANO KWA MSINGI WA MAENDELEO

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Watumishi wa serikali wamekumbushwa kuzidi kushirikiana,  kuaminiana, kushauriana na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ikiwemo matumizi ya mitandao sahihi inayokubalika serikalini katika kutuma taarifa.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha 6 cha  mamlaka ya serikali mtandao eGA Jijini Arusha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete amesisitiza watumishi wa kuziamini na kuzitumia taasisi za serikali kupata huduma ikiwemo huduma za kifedha na kuepuka kukopa taasisi za mikopo ya kausha damu.


Aidha ametoa rai kwa waajiri kuacha tabia ya kuwaondoa watumishi ofisini, badala yake ameelekeza uahirikiano na kila mmoja kutimiza wajibu wake,"Ndani ya Idara au taasisi kuna walioajiriwa kupitia mfumo wa ajira lakini kuna wale walioteuliwa, hapa nasisitiza mkafanye kazi kwa ushirikiano na wote mna haki sawa"

 Sambamba na hayo Waziri Kikwete amepongeza juhudi za dhati za mamlaka ya serikali mtandao eGA kwa kuharakisha huduma mbalimbali serikalini na kufanya mifumo kusomana. Amesisitiza watumishi kupewa nafasi ya kuendelea kusoma katika vyuo vilivyopo ndani na nje ya nchi ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani.


"TEHAMA inabadilika kila siku, lazima mjifunze kila wakati ili kuwa wabobezi, pia igeni mfano wa nchi zilizoendelea kama Indonesia na nchi za umoja wa  Kiarabu EU ambazo zimekuwa zikifanyiwa majaribio ya mifumo yao na wataalamu wa TEHAMA ili kubaini  kama iko sawa au imehakiwa. Kazingatieni na kufanyia kazi maazimio mliyojiwekea leo ili mkikutana mwakani muwe na majibu ya maswali yenu" amesema Waziri Kikwete.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa serikali mtandao nchini Eng.Benedict Ndomba amesema maazimio saba yaliyowekwa yatafanyiwa kazi sawasawa kwalengo la kuleta mapinduzi ya teknolojia na huduma bora kwa wananchi.

"Mamlaka itaendelea  kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kwa lengo la kuleta mapinduzi na mageuzi katika sekta hiyo na kufikia lengo la dira ya mwaka 2050"amesema Eng.Ndomba.

Mkurugenzi mkuu wa bodi sukari nchini Prof.Keneth Bengesi amepongeza mafanikio ya serikali mtandao nchini, na kusaidia taasisi mbalimbali kurahisisha majukumu yake ya utoaji huduma kwa wananchi.

"Kwetu Bodi ya sukari matumizi ya TEHAMA yamekuwa mkombozi mkubwa, ikumbukwe kuwa sisi ndio wenye jukumu la kuagiza sukari nje ya nchi, imetusaidia kutambua vibali feki na sahihi, kuokoa muda, kuokoa rasilimali fedha, kuongeza uwajibikaji na uwazi" ameeleza Prof.Bengesi.

Kikao hicho cha sita kimehudhuriwa na washiriki takribani 1400 na kubeba kaulimbiu "Kuboresha Utendaji Wa Serikali Kwa Kuimarisha Utoaji Wa Hudma Za Umma Kupitia Mifumo Salama Na Jumuishi ya Serikali Mtandao".

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post