Madereva wa pikipiki amabo ni Maafisa usafirishaji katika Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuacha tabia ya kushindana kukimbiza Pikipiki barabarani.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa hivyo ni vitendo hatarishi Kwa usalama wao pamoja na watumiaji wengine wa barabara kwani vitendo hivyo vinaweza kusababisha ajali barabarani.Sajenti Ndimila amewataka Maafisa usafirishaji hao kuacha tabia ya kuwekeana dau la pesa na Kisha kuingia barabarani kushindana kukimbiza Pikipiki ili mshindi apate pesa hizo kwani hayo mashindano sio rasmi na yanaweza kugharimu maisha yao pia kugharimu maisha ya watumiaji wengine wa barabara.Aidha Maafisa usafirishaji hao wametakiwa kujikanya wao Kwa wao endapo Kutakuwa na baadhi Yao wakifanya vitendo hatarishi barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima ambazo zinaweza kuepukika.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment