
Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, akifungua kikao.
Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya kata wilayani Mpanda wametakiwa kuongeza juhudi katika kusimamia uhai wa jumuiya, kuibua miradi ya maendeleo na kuimarisha utendaji wao.
Wito huo umetolewa Machi 30, 2026 na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka, wakati akifungua kikao cha kawaida cha makatibu hao kilichoanza saa 4:00 asubuhi.
Akizungumza katika kikao hicho, Maduka aliwataka makatibu kuwa watulivu na makini katika kujadili ajenda mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika kufanikisha majukumu ya jumuiya.
Katika tathmini ya vikao na matukio ya mwaka 2025, wajumbe walieleza kuridhishwa na utekelezaji wa majukumu, wakibainisha kuwa hakukuwa na changamoto kubwa zilizojitokeza katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama.
Kuhusu uhai wa jumuiya, Maduka aliwahimiza makatibu kuendelea kuhamasisha wanachama kulipa ada na kuandikisha wanachama wapya katika ngazi za matawi, mashina na kata ili kuimarisha jumuiya hiyo.
Aidha, aliwataka viongozi hao kufanya vikao vya mara kwa mara vya kikanuni pamoja na kuhakikisha wanatunza kumbukumbu sahihi za vikao na taarifa za wanachama kwa ajili ya rejea.
Katika ajenda ya miradi, makatibu walielekezwa kuibua na kuendeleza miradi ya kiuchumi itakayoongeza mapato ya jumuiya. Pia walitakiwa kuhakikisha miradi iliyopo inafufuliwa na kuendelezwa kwa lengo la kuimarisha uchumi wa jumuiya hiyo.
Maduka alisisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kuiboresha shule ya sekondari na ufundi ya Milala iliyopo Kata ya Misunkumilo, akibainisha kuwa hatua zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha eneo la shule linapimwa na kupata hati miliki, hatua itakayosaidia kuvutia uwekezaji.
Kikao hicho pia kilijadili maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yanayotarajiwa kufanyika Mei 7, 2026, ambapo makatibu walitakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kufanikisha shughuli hiyo.
Sambamba na hilo, viongozi hao walihimizwa kuendeleza umoja, mshikamano, nidhamu na ushirikiano ili kuhakikisha jumuiya inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Katika hatua nyingine, makatibu waliagizwa kufanya ziara katika kata na matawi kwa lengo la kuhamasisha uandikishaji wa wanachama, ulipaji ada pamoja na kutoa elimu na mafunzo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali.
Kikao hicho kilihitimishwa saa 7:00 mchana, ambapo viongozi walishukuru kwa ushiriki na michango ya mawazo iliyolenga kuboresha utendaji wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.
Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, akitoa maelekezo na kuongoza mjadala wakati wa kikao cha makatibu wa kata kilichofanyika Machi 30, 2026.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi kata ya Kakese, Manispaa ya Mpanda, Ndg. Maganga akichangia ajenda katika kikao cha makatibu wa Jumuiya ya Wazazi kata.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Mpanda, Ndg. Maziku, akichangia agenda katika kikao hicho.
Mh. Diwani wa Kata ya Ibindi, Ndg. Matongo, akiwasalimia makatibu wa Jumuiya ya Wazazi katika kikao chao kilichofanyika Machi 30, 2026, huku akisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu ya Jumuiya ya Wazazi na CCM kwa ujumla.
Mh. Diwani wa Kata ya Mtapenda, Halmashauri ya Nsimbo, Ndg. Anthony, akiwasalimia makatibu wa Jumuiya ya Wazazi kata katika kikao chao kilichofanyika Machi 30, 2026, huku akiwahimiza kuendeleza umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu ili kuongeza ufanisi na weledi wa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment