" Millioni Nane za Aweso zasomesha Vijana 80 wa Hamasa VETA

Millioni Nane za Aweso zasomesha Vijana 80 wa Hamasa VETA

Na: Mwandishi Wetu, PanganiWaziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani mkoani Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumaa Aweso, ameacha alama katika maisha ya vijana 80 wa Hamasa na Itifaki wa CCM wa wilayani Pangani baada ya kugharamia ada ya masomo yao kwa kulipa shilingi 8,220,000 kwa mwaka wa kwanza wa masomo yao ili kusoma kozi mbalimbali za ufundi katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha wilayani Pangani.Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Aweso, Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa, amesema Aweso ameguswa na vijana hao ambao wanajitolea kufanya shughuli mbalimbali za Chama kwa moyo wa uzalendo, hivyo ameamua kusaidia kutimiza ndoto zao za maisha kwa kugharamia ada ya mafunzo yao VETA."Mbunge wetu Jumaa Aweso ana upendo sana na vijana, kwa muda mrefu vijana wa Hamasa na Itifaki wamejitolea kufanya kazi za Chama bila malipo, hivyo katika kutambua mchango wao, Mbunge ametoa Milioni Nane Laki Mbili na Elfu Ishirini ili zilipe ada katika Chuo cha VETA Pangani ili wapate ujuzi waajiriwe na wengine wajiaji wenyewe," amesema Mkalipa.Mkalipa amewahimiza vijana hao 80 waliopata ufadhili huo kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na pia wasimuangushe mfadhili wao kwani vijana wengi wanatamani kupata fursa kama hiyo lakini wameikosa. Katika hatua nyingine, vijana hao wa Hamasa na Itifaki kutoka Kata zote 14 za wilaya ya Pangani, wamemshukuru Aweso kwa kujitolea kuwasomesha miaka yote miwili ya masomo yao huku wakiahidi kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao za maisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post