" MITANDAO YA KIJAMII INAVYO ATHIRI MAISHA YA VIJANA

MITANDAO YA KIJAMII INAVYO ATHIRI MAISHA YA VIJANA

Na Milu Malimi, Misalaba Media

Baadhi ya vijana kutoka mitaa mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga wameeleza namna wanavyoathirika na matumizi ya mitandao ya kijamii, wakibainisha kuwa hali hiyo inaendelea kuwa changamoto kubwa katika maisha yao ya kila siku.

Wakizungumza na Misalaba Media leo Machi 31, 2026, vijana hao wamesema matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii yamechangia kuongezeka kwa vitendo hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, hali inayosababisha kupungua kwa nguvu kazi ya taifa na kudhoofisha maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Baadhi ya vijana hao, akiwemo Heri Mlawa, Yohana Edward, Giles Yona na Yusufu Michael, wameeleza kuwa vijana wengi hutumia muda mwingi mtandaoni badala ya kujishughulisha na masomo au kazi, jambo linaloathiri maendeleo yao binafsi.

Aidha, wamebainisha kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yamepunguza mawasiliano ya ana kwa ana, kwani vijana wengi hupendelea kuwasiliana kupitia simu kuliko kukutana moja kwa moja, hali inayoweza kudhoofisha uhusiano wa kijamii na kifamilia.

Hata hivyo, vijana hao wameeleza kuwa mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa katika maisha yao endapo itatumika kwa malengo sahihi, wakisisitiza umuhimu wa kuitumia kwa kiasi na kwa busara ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa ujumla, wametoa wito kwa vijana wenzao kutumia teknolojia hiyo kwa manufaa, huku wakiepuka matumizi mabaya yanayoweza kuathiri mustakabali wao na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post