" MKAKATI ARUSHA KUJENGWA KWA NJIA NANE

MKAKATI ARUSHA KUJENGWA KWA NJIA NANE


_RC Makalla asisitiza utekelezaji yakinifu_

_TARURA  yataja changamoto_

Na, Egidia Vedasto, 

Misalaba Media, Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha na mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara mkoa CPA Amos Makalla amehimiza suala la  ujenzi wa miundombinu ya barabara kupewa kipaumbele kufuatia ugeni mkubwa wa Mabunge Duniani unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.

Amezungumza hayo katika kikao cha kwanza cha bodi ya barabara na kusisitiza uahirikiano na uwajibikaji ili kufikia mafanikio hayo.

"Nafasi hii mliyoipta Wabunge kuhudhuria kikao hiki itumieni vizuri, mkatusaidie kuelezea  changamoto zilizobainishwa na kuzipatia ufumbuzi".

Awali akizungumza na kikao hicho, Waziri wa habari, utamaduni  sanaa na michezo na Mbunge wa Arusha  Paul Makonda amesema umefika wakati sahihi wa kujenga barabara kwa njia nane.

Amesema"Naamini hili linawezekana, kinachotakiwa ni watu walipwe fidia kupisha upanuzi wa barabara hususan zinazoelekea uwanja wa AFCON na kutokea KIA kwenda Ngorongoro.  Tushirikiane kuangalia namna ya kufanikisha hili, kwa sasa mikutano yote mikubwa imeelekezwa hapa Arusha, mwezi wa nane wataingia Wabunge 2000 kutoka dunia nzima, lakini 2027 mashindano ya AFCON yatafanyika hapa, natoa wito kwenu TANROADS na TARURA kwa pamoja tuhakikishe suala la miundombinu linakaa sawa" 

Katika namna hiyo hiyo Meneja TARURA mkoa wa Arusha Eng.Nicholas Francis amebainisha changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na  msongamano hasa maeneo ya katikati ya Jiji (CBD), uharibifu wa miundonbinu ambao ni wizi wa alama za barabarani, kingo za madaraja, kutupa taka katika mifereji ya maji na barabara na kukata barabara bila kufuata utaratibu.

Changamoto zingine ni kilimo ama matumizi mabaya ya hifadhi za barabara kinyume cha sheria na kupitisha mifugo barabarani kinyume cha sheria ya barabara ya mwaka 2007 Na. 13 ya 2007 na kanuni zake za 2009.

"Kwa mwaka wa fedha 2026/2027 TARURA Mkoa wa Arusha umependekeza jumla ya Tsh Bilioni 19, 303, 251, 413.8 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja.Wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA mkoa wa Arusha unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya km 5752.834, madaraja 107 na makaravati 2639 kwa wilaya zote sita", 

"Katika mtandao huu wa km 5752.47 kati ya hizo barabara za lami km 170.407 (2.96%), barabara za changarawe km 1591.267 (27.66%) na barabara za udongo km3991.160 (69.38%)" amefafanua Eng.Nicholas.

    

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post