" RAIS SAMIA AMUASILI MTOTO ALIYETELEKEZWA TABORA

RAIS SAMIA AMUASILI MTOTO ALIYETELEKEZWA TABORA

 
Rais  Samia Suluhu Hassan, akiwa amembeba mtoto aliyemuasili.

Picha: Ikulu
Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa amembeba mtoto aliyemuasili.

Rais Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu katika makazi yake ya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo, Machi 11, 2026.

Mtoto huyo alitelekezwa awali katika mji wa Nzega mkoani Tabora na baadaye kukabidhiwa kwa Rais na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, mtoto huyo aliokotwa Januari 17, 2026 karibu na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini. Baada ya kupatikana, alichukuliwa kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi Tanzania na kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Akimpokea mtoto huyo, Rais Samia ameahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

Aidha, Rais amewataka wananchi kuepuka tabia ya kutupa watoto na badala yake kuwapeleka katika mamlaka za kisheria au vituo vya kulelea watoto ili kuhakikisha wanapata ulinzi na malezi stahiki.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. 

“Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” amesisitiza Rais Dk Samia.

Post a Comment

Previous Post Next Post