" RAIS WA IPU DKT. TULIA AONGOZA MKUTANO MAALUM WA IPU NA UN NCHINI MAREKANI

RAIS WA IPU DKT. TULIA AONGOZA MKUTANO MAALUM WA IPU NA UN NCHINI MAREKANI

 

Na mwandishi wetu Misalaba media 

Machi 11, 2026, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb), ameongoza mkutano maalum uliojadili hali ya usawa wa uongozi kwa wanawake. Mkutano huo ulifanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, katika ukumbi wa ECOSOC, New York, Marekani.

Hafla hiyo ya kibunge iliandaliwa na Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa kushirikiana na UN Women, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake.

Aidha, mkutano huo ulijadili pia nafasi na jukumu la mabunge katika kufikia usawa katika maamuzi ya uongozi, pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.





Post a Comment

Previous Post Next Post