Na Milu Malimi, Misalaba Media
Baadhi ya vijana kutoka mitaa mbalimbali katika
Manispaa ya Shinyanga wameeleza jinsi wanavyoathirika na changamoto ya ukosefu
wa ajira, wakibainisha kuwa hali hiyo inaendelea kuwa kikwazo kikubwa katika
maisha yao ya kila siku.
Wakizungumza na Misalaba Media leo Machi 27, 2026,
vijana hao wamesema ukosefu wa ajira umechangia kuongezeka kwa vitendo
visivyofaa ikiwemo ulevi, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kupoteza nguvu
kazi ya taifa, hali inayodhoofisha maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Baadhi ya vijana hao, akiwemo Magreth Charles,
Zephania Lucas na Joseph Steven, wameeleza kuwa kutokana na hali hiyo, wengi
wao hulazimika kujishughulisha na kazi ndogondogo kama bodaboda na ujasiriamali
mdogo, ambazo mara nyingi hazikidhi mahitaji yao ya msingi ya kila siku.
Vijana hao pia wameiomba serikali pamoja na sekta
binafsi kuongeza uwekezaji utakaowezesha upatikanaji wa mikopo na kuboresha
mazingira ya biashara, ili kuwasaidia vijana kuanzisha shughuli zao na
kujiajiri.
Aidha, wameitaka serikali kuondoa vikwazo
vinavyokwamisha biashara ndogondogo na kuongeza fursa za uwekezaji kwa vijana,
huku wakisisitiza umuhimu wa kutoa mafunzo ya ujuzi wa kazi ili kuwajengea
uwezo wa kujitegemea.
Kwa upande mwingine, wamezitaka mamlaka husika,
viongozi pamoja na wadau wa maendeleo kuchukua hatua za haraka kukabiliana na
changamoto ya ajira kwa vijana, ikiwa ni pamoja na kupanua fursa za mafunzo na
kuweka mazingira rafiki ya kuanzisha na kukuza biashara.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment