Na mwandishi wetu Misalaba media.
Mbeya
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wamejengewa uwezo kwenye mafunzo maalum wa mfumo wa kielektroniki wa Tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma(PEPMIS) lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa umma.
Mafunzo haya yamezinduliwa leo Machi 25, 2026 katika ukumbi wa Sapanjo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga huku akiwataka watumishi wa Wilaya ya Chunya kuzingatia taratibu za utumishi wa umma kwa kutoa huduma bora na zenye ufanisi pamoja na kulinda hadhi ya mtumishi wa umma.
“Sisi watumishi wa umma tunaangaliwa katika kila nyanja kwenye jamii, sisi ndio suhuluhisho la matatizo ya jamii, wananchi wataipenda au kuichukia serikali kupitia kwako mtumishi wa umma kwakuwa wewe ndio taswira ya serikali” amesema Mhe. Batenga.
Aidha Mhe. Batenga aliwataka washiriki wa mafunzo kuitumia vyema semina hiyo kwa kufanya kazi alizopangiwa bila kudanganya kwenye kujaza taarifa za utendaji kazi kwenye mfumo kwakuwa kazi halisi iliyofanyika haijifichi.
“Hii semina ni nzuri sana kwasababu watumishi wanahitaji kukumbushwa namna bora ya kufanya majukumu yao ya kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na matokeo chanya” amesema Mhe. Batenga.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Dkt. Lucas Theodory, Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira, amesema mafunzo ya leo tumejifunza zaidi namna ya kufuata itifaki ya kupokea viongozi, kufanya tathmini ya kielektroniki kwa watumishi walio chini yangu pamoja na kujifunza jinsi ya kufanya uwekezaji kupitia mfumo (e-wekeza).
Kwa upande wake, Ridhiwani Mshighati, afisa rasilimali watu amesema mafunzo yalikuwa na tija kwa kuwa yamekuja wakati muafaka haswa kwenye mfumo wa (e-wekeza) ambapo watumishi watafanya uwekezaji na kuepukana na changamoto ya kifedha na kuimarisha Uchumi wa mtumishi mmoja mmoja.
Mada mbalimbali zilitolewa katika semina hiyo ikiwemo, mafunzo ya tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma, somo kuhusu itifaki na uwekezaji kielektroniki yametolewa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, utumishi wa umma yakilenga kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa umma na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment