" WAZIRI ULEGA AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA UFANISI

WAZIRI ULEGA AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA UFANISI


Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, akizungumza na watumishi wa Wizara ya Ujenzi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi jijini Dodoma, Machi 30, 2026.

Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amezitaka taasisi zote zilizo chini ya Wizara hiyo zinapaswa kuongeza uwajibikaji, nidhamu na ufanisi wa kazi ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.

Aidha, amelipongeza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi kwa kuendelea kudumisha ushirikiano mzuri kati ya menejimenti na watumishi, jambo ambalo limechangia kuimarika kwa utendaji kazi na kuepusha migogoro mahala pa kazi.

Akizungumza Machi 30, 2026, jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Ulega amesema kuwa taarifa za utendaji wa bodi za taasisi zinapaswa kuwasilishwa kwa wakati, huku akibainisha kuwa kisheria ripoti hizo zinatakiwa kuwasilishwa miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha.

Aidha, Mhe. Ulega amebainisha kuwa viongozi wa taasisi zinazotekeleza mageuzi wanatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ili kufikia malengo yaliyowekwa. Alitaja mfano Wakala wa Majengo Tanzania, akieleza kuwa umeelekezwa kuandaa mpango wa biashara (Business Plan) utakaoiwezesha taasisi hiyo kujiendesha kibiashara.

Aidha, Mhe.Ulega amesema kuwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) unapaswa kuongeza juhudi za kusimamia miradi ya barabara na viwanja vya ndege ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Vilevile, taasisi zinazokusanya maduhuli, zikiwemo AQRB, ERB na CRB, zinatakiwa kuongeza makusanyo na kudhibiti matumizi ili kuboresha ufanisi.

Aidha, Waziri Ulega amebainisha kuwa viongozi wanapaswa kuzingatia maadili ya uongozi wa umma kwa kupiga vita rushwa, kuheshimu utawala wa sheria na kutunza siri za ofisi, akisisitiza kuwa nafasi walizonazo ni dhamana kwa wananchi. “Ni wajibu wenu kuhakikisha rasilimali za umma zinatumiwa kwa uadilifu na weledi ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema kuwa.

Aidha,Mhe. Ulega amesema kuwa ni muhimu kuitisha mabaraza ya wafanyakazi katika taasisi zote ili kuimarisha mawasiliano kati ya menejimenti na watumishi, huku akibainisha kuwa bado kuna malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi. Watumishi wa sekta ya ujenzi amesema kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, kuepuka vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali za ofisi, ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.Awali akizungumza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mha. Aisha Amour, amebainisha kuwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi unajadili mafanikio na changamoto za utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/26, pamoja na maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27. Aidha, amebainisha kuwa Wizara imefanikiwa kutoa ajira mpya kwa watumishi 50, uthibitisho wa watumishi 12, kupandishwa vyeo, mafunzo kwa kadri ya watumishi 346, pamoja na maslahi mbalimbali yenye jumla ya Shilingi milioni 350 kwa watumishi 18, ikiwemo posho za kazi za ziada, malipo ya safari za kikazi, gharama za uhamisho, likizo, matibabu na mikopo.  

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post