
Aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Endasaboghechan, wilayani Hanang’, Bw. Juma Raphael Iddi, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hanang’ akikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka.
Shauri hilo la jinai namba 8355/2026 lilifunguliwa Aprili 20, 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mh. Arnold Kileo.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka kutoka TAKUKURU Wilaya ya Hanang’, Bw. Daudi Kingazi, umeeleza mahakama kuwa mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo katika nyakati tofauti mwaka 2023. Inadaiwa kuwa alighushi saini za watia saini wa shule hiyo katika hati za malipo pamoja na hundi mbalimbali na kisha kutoa fedha benki.
Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka chini ya vifungu vya 333, 335(d)(i) na 337 vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16.
Baada ya kusomewa hati ya mashtaka, mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo.
Mahakama imempa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa, ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka serikali za mitaa na kusaini bondi ya Shilingi milioni mbili kila mmoja.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Mei 5, 2026 kwa ajili ya kusomwa kwa hoja za awali (PH).
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment