NA: MWANDISHI WETU - PANGANIShirika la AMREF kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ireland, limefanikisha upatikanaji wa Simu Janja 102, ambazo zimekabidhiwa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Pangani ili ziboreshe utoaji wa huduma bora kwa wananchi.Makabidhiano hayo yamefanyika Aprili 15, 2026, mbele ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Wakili Agape Fue, ambapo vifaa hivyo vinatarajiwa kuwezesha mawasiliano yahusuyo majanga ma milipuko ya magonjwa.Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ni wadau muhimu katika kufanikisha utoaji wa taarifa za maendeleo ya afya katika kaya mbalimbali ambapo mawasilino ni nyenzo muhimu, yenye kuwezesha ufuatiliaji na kudhibiti ueneaji wa mgonjwa na kuepusha athari kubwa ambazo zingeweza kutokea baadaye.Wakili Fue amelishukuru Shirika la AMREF kwa kuwezesha vifaa hivyo ambavyo ameahidi vitatumika ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu ya wahudumu hao wa afya."Teknolojia ni muhimu, simu hizi zitaongeza kasi ya upashaji taarifa muhimu za afya na hivyo hatua stahili zitachukuliwa kwa wakati ili kuboresha afya za wananchi wetu," amesema Wakili Fue.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment