" ASKOFU MWASOVYE AKANUSHA TAARIFA ZA WAUMINI KUMKATAA MCHUNGAJI MBALIZI, ASEMA NI UZUSHI NA UPOTOSHAJI

ASKOFU MWASOVYE AKANUSHA TAARIFA ZA WAUMINI KUMKATAA MCHUNGAJI MBALIZI, ASEMA NI UZUSHI NA UPOTOSHAJI


Na Lydia Lugakila-Misalaba media 

Mbeya

Askofu wa Jimbo la Mbeya, Elly Mwasovye wa Kanisa la Pentecostal Hollness Asstion Mission Tanzania (PHAMT), amewatoa hofu wananchi kufuatia taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari zikidai kuwa waumini wa kanisa hilo lililopo Mbalizi, mkoani Mbeya, walimkataa mchungaji mpya Frans Mwambigija.

Akizungumza na vyombo vya habari, Askofu Mwasovye amesema kuwa taarifa hizo si za kweli, na ni upotoshaji uliolenga kuleta taharuki miongoni mwa waumini na jamii kwa ujumla.


 Alieleza kuwa Mchungaji Mwambigija alisimikwa rasmi tarehe 12 Aprili mwaka huu kwa mujibu wa katiba ya kanisa hilo, ili kuendelea na jukumu la kuliongoza.


Askofu huyo alisisitiza kuwa yeye ni miongoni mwa viongozi waliokuwepo wakati wa ibada ya usimikaji, na kwamba ibada hiyo ilifanyika kwa amani, furaha na utulivu mkubwa bila ya kuwepo kwa vurugu yoyote kama ilivyoripotiwa.

Aliongeza kuwa viongozi wa kanisa hilo wamekutana na kujadili taarifa hizo na kubaini kuwa si za kweli.


Amesema kuwa kazi ya kumsimika mchungaji ni ya Mungu, na yeyote anayesambaza taarifa za uongo dhidi ya kazi hiyo atahukumiwa na Mungu kwa haki.

Kwa upande wao, baadhi ya waumini wa kanisa hilo walihojiwa na vyombo vya habari, ikiwemo misalaba media, na wote walikanusha kuwepo kwa tukio la kumkataa mchungaji huyo, wakisema ibada ilifanyika kwa utulivu na mshikamano mkubwa.

Naye Mchungaji Frans Mwambigija, aliyesimikwa rasmi, alithibitisha kuwa hakukuwa na tukio lolote la vurugu au upinzani kutoka kwa waumini. 

Alifafanua kuwa hakuna mali ya kanisa iliyochukuliwa wakati wa ibada hiyo.

Hata hivyo, alieleza kuwa siku ya Jumanne, Aprili 13, aliyekuwa shemasi wa kanisa hilo, Maendeleo Mwakapiki, alifika kanisani hapo akidai ametumwa na aliyekuwa mchungaji mstaafu, Christopher Mwakindu, kuchukua kiti na meza ambayo ilikuwa mali yake binafsi. Uongozi wa jimbo uliridhia kuchukuliwa kwa vifaa hivyo baada ya kubaini kuwa si mali ya kanisa bali ya mchungaji mstaafu.


Kwa ujumla, viongozi wa kanisa hilo wamewataka wananchi kupuuza taarifa hizo zisizo na ukweli na kuendelea kudumisha amani na mshikamano.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post