" WANAUME WAHIMIZWA KUCHUKUA NAFASI KATIKA MALEZI YA AWALI YA MTOTO

WANAUME WAHIMIZWA KUCHUKUA NAFASI KATIKA MALEZI YA AWALI YA MTOTO

 

Na Lydia Lugakila-Misalaba media 

Mbeya

Wajumbe wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMAM) wamejipanga kuhakikisha wanawahamasisha wanaume kushiriki katika mambo mbalimbali yanayohusu malezi na makuzi ya watoto, kwani jukumu la malezi ya mtoto ni la wazazi wote—baba na mama.


Hayo yamezungumzwa Aprili 14 2026, wakati wa kikao cha robo ya tatu cha Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya.

Wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana kuhakikisha wanatumia majukwaa mbalimbali kuelimisha jamii, hususan wanaume, kushiriki kikamilifu katika masuala ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga familia bora inayozingatia afya, lishe, ulinzi na usalama wa mtoto, malezi yenye mwitikio pamoja na fursa za awali za ujifunzaji.


Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bi Lutness Mbisa, ametoa msisitizo kwa wajumbe wa kikao hicho kuhakikisha wanayafanyia kazi yote yaliyojadiliwa, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutekeleza majukumu yao na kuandaa taarifa kwa wakati ili kurahisisha utendaji kazi.


“Niwaombe wajumbe tuzingatie yote tuliyokubaliana katika kikao hiki, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa kwa wakati. Lakini pia jukumu la kuelimisha jamii katika majukwaa mbalimbali ni la kwetu sote, hivyo tukayafanyie kazi yale yote tuliyokubaliana, pamoja na kushughulikia mapungufu tuliyoyabaini,” amesema Mbisa.


Aidha, kikao kimejadili na kupitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu yanayolenga Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. 

Taarifa hizo zimesomwa na wajumbe kutoka idara za Afya, Maendeleo ya Jamii na Elimu ya Msingi ili kutathmini hali ya utekelezaji, changamoto na mafanikio yaliyopatikana.

Kikao hicho kimehusisha wajumbe mbalimbali, wakiwemo wadau wanaotekeleza miradi inayolenga watoto, waratibu kutoka idara ya Elimu ya Msingi, Maendeleo ya Jamii pamoja na Afya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post