" ASKOFU NYAISONGA AHIMIZA MATENDO MEMA KIPINDI CHA PASAKA

ASKOFU NYAISONGA AHIMIZA MATENDO MEMA KIPINDI CHA PASAKA

Na Lydia Lugakila-Misalaba Media, Mbeya

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya, Gervaz Nyaisonga, amewahimiza waumini wa Kanisa Katoliki kufanya matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu na kujitoa ili kuishi katika upya, hasa katika kipindi hiki cha Pasaka.

Askofu Nyaisonga ametoa wito huo Aprili 2, 2026, kuelekea Siku Kuu ya Pasaka kupitia salamu zake kwa Watanzania, zilizoambatana na wito kwa waamini wake.

Amesema katika kipindi cha Pasaka, waumini wanapaswa kuendeleza matendo mema, kusaidiana wakati wa dhiki, kusameheana pale wanapokoseana, pamoja na kutubu dhambi.

Aidha, ameongeza kuwa Yesu aliwapenda waamini kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kujibu upendo huo kwa kumpenda Mungu kwa moyo wote kama anavyotupenda. 

Pia amewatakie heri ya Pasaka waumini hao na Watanzania kwa ujumla.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post