" BODABODA SHINYANGA WASISITIZA KULINDA AMANI, WAKATAA KUINGIZWA KWENYE VURUGU

BODABODA SHINYANGA WASISITIZA KULINDA AMANI, WAKATAA KUINGIZWA KWENYE VURUGU


Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa Maafisa Usafirishaji Wilaya ya Shinyanga, Mohamed Juma, amesisitiza umuhimu wa kulinda amani, akieleza kuwa ni msingi mkubwa wa shughuli za kila siku hususan kwa vijana wanaojihusisha na kazi za usafirishaji kama bodaboda.

Akizungumza na Misalaba Media, Mohamed amesema kuwa bila amani, vijana wengi hawawezi kufanya kazi zao za kujipatia kipato, akitolea mfano wa waendesha bodaboda ambao hutegemea utulivu wa mazingira ili kuendesha shughuli zao kwa uhuru na usalama.

“Amani ni suala la msingi kuliko kitu chochote, kwa sababu kama hakuna amani huwezi kutoka kwenda kuendesha bodaboda,” amesema.

Ameongeza kuwa katika tukio la maandamano yaliyotarajiwa kufanyika tarehe 29 mkoani Shinyanga, hakukutokea vurugu yoyote kutokana na msimamo wa vijana waliokataa kushiriki vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama.

Amesema walikubaliana kwa pamoja kutoruhusu kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa au watu wachache wenye nia ya kuvuruga amani, akibainisha kuwa hawako tayari kujiingiza kwenye migogoro kwa maslahi ya wengine.

“Hatuko tayari kudanganywa na wanasiasa au wahuni wachache ili sisi tuumie, wakati wao wanaendelea na maisha yao,” ameongeza.

Mohamed ametoa rai kwa vijana kuendelea kuwa walinzi wa amani, kuepuka kushawishika na fedha au ahadi zisizo na tija, na badala yake kujikita katika shughuli halali za kujipatia kipato.

Amesisitiza kuwa kulinda amani ni jukumu la kila mmoja, na kwamba jamii ikidumisha utulivu itaendelea kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa vijana na taifa kwa ujumla.

 

Mwenyekiti wa Maafisa Usafirishaji Wilaya ya Shinyanga, Mohamed Juma.

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post