NA: MWANDISHI WETU - DODOMA Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Mary Chatanda, ameshiriki msimu wa tatu wa mbio za hisani za "Bunge Marathon," zilizofanyila Aprili 18, 2026, Jijini Dodoma.Akizungumzia mbio hizo, Chatanda ameupongeza uongozi wa Bunge, wadhamini kwa kuandaa mbio hizo zenye lengo la kukuza umoja, mshikamano, kujenga afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza."Mbio za Bunge Marathon zinawaleta viongozi na wananchi pamoja, jambo linalojenga umoja na mshikamano wa Kitaifa. Tukumbuke pia mazoezi ni afya, hivyo kadri tunavyoshiriki tunajenga afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiathiri wananchi wengi," amesema Chatanda.Bunge Marathon huratibiwa na uongozi wa Bunge na huwashirikisha wabunge, viongozi, wadau na wananchi kushiriki kukimbia umbali wa Kilometa 5, 10 na 21, huku washindi wa mbio hizo wakizawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment