Diwani wa Kata ya Butobela, Wilaya ya Mbogwe mkoani
Geita, Paschal maarufu kama “King Mapungo”, ameshiriki katika mkutano mkuu wa
kawaida wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika katika ofisi mpya za chama mkoani
humo, ukiwa na lengo la kuwasilisha mafanikio ya uongozi wa mkoa ndani ya
kipindi cha miaka minne.
Katika mkutano huo, viongozi na wanachama walipata
fursa ya kuelezwa utekelezaji wa majukumu mbalimbali yaliyofanywa chini ya
uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Nicholaus Kasendamila, ambapo hatua
mbalimbali za maendeleo ya chama na jamii ziliwasilishwa.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Paschal “King
Mapungo” alieleza kuridhishwa na mwenendo wa uongozi wa chama katika kipindi
hicho, akibainisha kuwa mafanikio yaliyopatikana yametokana na ushirikiano
mzuri wa viongozi na wanachama.
Alisema ni muhimu kuendeleza mshikamano na kuongeza
juhudi katika kutekeleza majukumu ya chama ili kuimarisha zaidi maendeleo
yaliyopatikana.
Mkutano huo ulifanyika kwa lengo la kuwapa wanachama mrejesho wa kazi zilizotekelezwa pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza chama katika ngazi ya mkoa na wilaya.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment