Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuheshimu vivuko vya reli ili kuepuka ajali za mara Kwa mara.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika kituo Cha Maafisa usafirishaji Cha Ally's star ambapo amewataka madereva hao kuheshimu vivuko vya reli Kwa kusimama na kujiridhisha hali ya kiusalama kabla ya kuchukua maamuzi ya kuvuka.Sajenti Ndimila amewaelimisha kwamba Treni inapaswa kupewa kipaumbele kwahiyo kila mmoja anawajibika kuheshimu vivuko hivyo kuepukana na ajali ambazo zinaweza kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu baada ya kuigonga Treni.Aidha Maafisa usafirishaji hao wametakiwa kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kupaza sauti zao Kwa kuwaelimisha watumiaji wengine wa vyombo vya moto ili kutokomeza matukio ya ajali kwenye vivuko vya reli.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment