" DIWANI MPOLI ATOA UJUMBE MZITO KWA WAHITIMU VANESSA SEKONDARI MBEYA

DIWANI MPOLI ATOA UJUMBE MZITO KWA WAHITIMU VANESSA SEKONDARI MBEYA

Na Lydia Lugakila-Misalaba Media MbeyaWahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Vanessa (2026), iliyopo Kata ya Isyesye, mkoani Mbeya, wamehimizwa kwenda mtaani na kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuharibu mustakabali wao na Taifa kwa ujumla.Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Isyesye, iliyopo Mkoani Mbeya Novatus Mpoli Augustino, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 8 ya shule hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule.Akizungumza katika hotuba yake, mhe. Mpoli amesema matarajio ya Serikali ni kuona wahitimu hao wanatumia elimu waliyoipata, hususan ya ufundi, kuleta mchango chanya katika jamii. Amesisitiza kuwa katika mazingira ya sasa, ujuzi na fani vina umuhimu mkubwa zaidi katika kujenga maisha bora.Aidha, kiongozi huyo ameonya dhidi ya tabia hatarishi akisema Serikali haitarajii kuona wahitimu wa Kidato cha Sita wakijihusisha na ulevi, matumizi ya dawa za kulevya au vitendo vingine vinavyoharibu taswira ya jamii. Badala yake, amewataka wawe mfano bora na kutafsiri elimu yao kwa vitendo ili jamii iweze kunufaika.Amewahimiza wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao, akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira wezeshi ya kupata mikopo ya elimu ya juu kwa wahitimu wote, bila ubaguzi kati ya wanafunzi wa shule za serikali na binafsi.Vilevile, mhe Diwani  yamewataka wahitimu kuwa wazalendo kwa Taifa lao na kuepuka kushiriki katika vitendo vya kulidhalilisha au kulizungumzia vibaya Taifa. Amesisitiza kuwa Tanzania ndiyo Nchi yao pekee na wanapaswa kuilinda na kuijenga.“Nendeni mkaielekeze jamii namna bora ya kulitumikia Taifa lao na kulipambania ili mtimize ndoto zenu,” alisisitiza Mpoli.Kwa upande mwingine, Diwani huyo ameipongeza Shule ya Sekondari Vanessa kwa juhudi zake za kuwahudumia watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Amesema shule hiyo inahudumia jumla ya wanafunzi yatima 66, ambapo 13 kati yao ni wahitimu wa mwaka huu.Ameongeza kuwa shule hiyo imekuwa zaidi ya taasisi ya elimu kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya ufundi kama vile kompyuta na ushonaji, huku ikiwa na mipango ya kuanzisha kozi za umeme na useremala ambapo pia imekuwa ikihamasisha shughuli za kilimo.Katika kuunga mkono juhudi hizo, Diwani Mpoli ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa shule Aidha, amepongeza uongozi wa shule chini ya Tehirah Foundation pamoja na Mkuu wa Shule, Exon Mwakalikamo, kwa uongozi bora uliosaidia kuifanya taasisi hiyo kuaminika.Naye Mkuu wa Shule hiyo, Exon Mwakalikamo, amesema jumla ya wahitimu wa Kidato cha Sita mwaka huu ni 42, wakiwemo wanafunzi yatima 13. Ameeleza kuwa awali watoto wengi yatima walikuwa mitaani, lakini kupitia ushirikiano na viongozi wa serikali za mitaa pamoja na vibali rasmi vya Serikali, waliweza kuwachukua na kuwasaidia kielimu kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Sita.Hata hivyo amesisitiza kuwa dhamira ya shule hiyo ni kuendelea kuwasaidia watoto wenye uhitaji ili waweze kufikia ndoto zao kupitia elimu.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post