" Fiston Mayele na Wenzake Mambo Safi, Rais Awapa Nyumba na Magari

Fiston Mayele na Wenzake Mambo Safi, Rais Awapa Nyumba na Magari

 

Fiston Mayele na Wenzake Mambo Safi, Rais Awapa Nyumba na Magari

Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamekabidhiwa zawadi ya magari na nyumba na Rais wa nchi hiyo kufuatia mafanikio ya timu hiyo kufuzu kucheza Kombe la Dunia. Zawadi hiyo imetolewa kama pongezi na kutambua juhudi za wachezaji baada ya kufanikiwa kuifunga Jamaica bao 1-0 katika mechi ya kufuzu.

 

DRC imefanikiwa kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Marekani, Canada na Mexico, na hivyo kuandika historia nyingine kwa soka la nchi hiyo. Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo, DRC imepangwa katika Kundi K pamoja na timu za Ureno, Colombia na Uzbekistan.

DRC inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Ureno Juni 17 mwaka huu, katika mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka wa nchi hiyo pamoja na Afrika kwa ujumla.

Serikali ya DRC imeeleza kuwa zawadi ya magari na nyumba kwa wachezaji ni sehemu ya kutambua mchango wao kwa taifa na kuhamasisha wanamichezo wengine kufanya vizuri wanapoliwakilisha taifa katika mashindano ya kimataifa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post