" FUNZO KWA VIJANA KUTOKA KATIKA OPERESHENI YA POLISI TANGA

FUNZO KWA VIJANA KUTOKA KATIKA OPERESHENI YA POLISI TANGA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kufanya operesheni kabambe na kuwaokoa vijana 87 waliokuwa wamenaswa katika mtego wa utapeli uliopambwa kwa ahadi za utajiri wa haraka kupitia biashara ya mtandaoni. 

Vijana hao, ambao walikuwa wakishikiliwa katika mazingira duni, wameokolewa kutoka katika mikono ya kampuni feki ya "Champions E-Commerce Education" iliyokuwa ikijipatia mamilioni ya fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika kile kinachoonekana kuwa somo chungu kwa vijana nchini, uchunguzi wa polisi umebaini kuwa kila mmoja wa vijana hao alilazimika kutoa kati ya Shilingi 600,000 hadi Shilingi milioni nne kama mtaji wa awali. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, ameeleza kuwa vijana hao waliaminishwa kuwa fedha hizo zingewapatia mafunzo na faida nono ndani ya muda mfupi, huku ukweli ukiwa ni mbinu ya kuwapora akiba zao.

Tukio hili linaakisi hali ya hatari wanayokumbana nayo vijana wengi wanaotafuta maisha kwa shauku kubwa bila kufanya uchunguzi wa kina. 

Licha ya kutoa kiasi kikubwa cha fedha, vijana hao walikutwa wakiishi katika mazingira yasiyoridhisha huku wakipewa mafunzo ya kisaikolojia yaliyolenga kuwapumbaza wasiweze kushtukia mchezo huo wa kitapeli. 

Jeshi la Polisi tayari limewatia mbaroni vijana wawili, Mohammed Idrisa (24) na Fidolini Rashidi (21), wanaotuhumiwa kuwa waratibu wa mtandao huo. 

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni ushindi kwa usalama wa raia, lakini ni onyo kwa vijana wengine wanaojihusisha na biashara za aina hiyo. Polisi wamesisitiza kuwa wataendelea kuwasaka wote wanaohusika na mitandao hii ya kitapeli inayolenga kunyonya nguvu kazi ya taifa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post