
Msanii wa Bongo Fleva Gaddy Shine amefunguka mengi
katika kipindi cha Misalaba Media, akieleza hatua aliyofikia kwenye safari yake
ya muziki pamoja na mipango yake ijayo. Gaddy Shine amesema kwa sasa anajiandaa
kuachia EP mpya itakayobeba nyimbo kadhaa alizozifanyia kazi kwa ubora mkubwa,
akiahidi mashabiki wake kupata burudani ya kiwango cha juu.
Ameongeza kuwa katika EP yake hiyo mpya, ameshirikiana
na wasanii mbalimbali akiwemo Beka Fleva pamoja na Bringt, akisisitiza kuwa
kazi hiyo italeta ushindani mpya na sura tofauti katika muziki wake.
Katika mazungumzo hayo, amekanusha vikali taarifa
zilizokuwa zikisambaa kuwa alikuwa chini ya Best Nasso, akifafanua kuwa msanii
huyo alimsaidia tu katika baadhi ya hatua za awali za muziki wake lakini
hakuwahi kuwa chini yake. Aidha, Gaddy Shine amegusia changamoto za baadhi ya
wasanii wenzake, akidai kuwa kuna wanafiki ndani ya tasnia hasa kutoka maeneo
aliyotokea, huku akieleza pia namna baadhi ya wasanii wakubwa wanavyoshindwa
kuthamini na kuheshimu sehemu walikotoka.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment