Na Moshi NdugulileViongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Mkoa wa Shinyanga wameonya vikali vitendo vya hujuma dhidi ya miundombinu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga, huku wakiahidi kutumia majukwaa ya kidini kukemea tabia hiyo.Onyo hilo limetolewa baada ya viongozi hao kutembelea mradi huo na kujionea hatua ya utekelezaji wake, ambapo ujenzi umefikia asilimia 97.3 ya ukamilishaji.Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamisi, alisema wataendelea kuhubiri amani na uzalendo kupitia nyumba za ibada ili kukomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundombinu ya umma.Alisema vitendo hivyo vinapaswa kupigwa vita kwa kuwa serikali inawekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote, akibainisha kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutafungua fursa nyingi za kiuchumi na kibiashara katika mkoa huo.Viongozi wa JMAT Mkoa wa Shinyanga wamesema utekelezaji wa mradi huo unaakisi kiwango cha juu cha ukomavu wa serikali katika kupanga, kuwekeza na kusimamia miradi ya maendeleo.Kwa upande wake, msimamizi wa uwanja huo, Lugano Mwinuka, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Athuman Mombokaleo, alisema mradi huo utakamilika hivi karibuni na utaimarisha huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya Shinyanga.Aliongeza kuwa uwanja huo utaongeza fursa za biashara, kukuza shughuli za kiuchumi na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali.Hata hivyo, Mwinuka alieleza kuwa pamoja na mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo, bado kuna changamoto ya wizi wa miundombinu. Alibainisha kuwa Januari mosi mwaka huu, watu wasiojulikana waliiba vyuma vya uzio wa uwanja huo, hali inayohitaji hatua kali za kukemea.Naye Mhandisi Chiyando Matoke, akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), alisema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 44.8, ambapo hadi sasa serikali imelipa shilingi bilioni 38.6 kwa mkandarasi.Mhandisi Matoke alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za kijamii nchini, ikiwemo mkoa wa Shinyanga.Aidha, alisema serikali tayari imelipa fidia kwa wananchi wote waliopisha utekelezaji wa mradi huo.Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na unatekelezwa na mkandarasi wa China, Hennan International Corporation Group Co. Ltd (CHICO)
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment