Moshi NdugulileViongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Mkoa wa Shinyanga wamekemea vikali tabia iliyozuka kwa baadhi ya watu ya kuzua taharuki kwa kudai kuibiwa sehemu zao za siri baada ya kuguswa au kushikwa begani, wakieleza kuwa ni imani potofu zinazochafua hali ya utulivu katika jamii.Wametoa kauli hiyo walipotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kumtia moyo na kumpa ushirikiano katika kukabiliana na matukio hayo. Ziara hiyo imekuja kufuatia matukio matatu yaliyohusisha vijana wawili waliopatikana na hatia ya kutoa taarifa za uongo na kuhukumiwa kifungo jela, baada ya kuzua taharuki wakidai kupoteza sehemu zao za siri kwa njia hizo.Viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis na Askofu Dkt Emanuel Makala wamesema vitendo hivyo ni uzushi unaolenga kuwawezesha watu wasio waadilifu kujipatia fedha kwa njia ya ulaghai.Wamesisitiza kuwa JMAT itaendelea kukemea vitendo hivyo kwani vinakinzana na maadili na vinaendeleza imani potofu katika jamii.Kwa upande wake, Mtemi Kidola wa II amesema hali hiyo ni ishara ya uhuni unaofanywa na baadhi ya vijana wanaotumiwa vibaya na watu wenye maslahi binafsi, wakirubuniwa kuzua taharuki kwa lengo la kujinufaisha.Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi, amewahakikishia viongozi hao kuwa, jeshi hilo linaendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote wanaobainika kuhusika na tuhuma za kuzua taharuki kwa madai ya kupoteza sehemu za siri.Amesema hadi sasa ni matukio matano yametokea wilayani Kahama, ambapo watuhumiwa wawili kati yao wamehukumiwa kifungo jela, huku akiiomba JMAT kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na vyombo vya dola katika kuelimisha jamii na kulinda amani. “JMAT ni Jumuiya ya Maridhiano na Amani inayowaleta pamoja viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali ya Kikristo na Kiislamu, ikijumuisha pia viongozi wa mila na desturi wakiwemo watemi na sungusungu. Lengo kuu la jumuiya hii ni kukuza umoja, maelewano, na mshikamano katika jamii kupitia majadiliano, usuluhishi wa migogoro, na kuimarisha amani endelevuMWISHO
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment