" JUMUIYA YA WAZAZI CCM MBEYA MJINI YAENDESHA ZOEZI LA UPANDAJI MITI

JUMUIYA YA WAZAZI CCM MBEYA MJINI YAENDESHA ZOEZI LA UPANDAJI MITI

 

Na Lydia Lugakila Misalaba Media,

Mbeya

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini, kwa kushirikiana na watengeneza maudhui mtandaoni ambaye ni MC Mboneke, Mr Mkazi na Mkurugenzi wa Wafanyakazi Comedy, Nox M, pamoja na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Mbeya Green City Club, mnamo April 21,2026 wameendesha zoezi la upandaji miti ya matunda na kivuli katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya.


Zoezi hilo limefanyika katika Shule ya Msingi Sistila, Ilemi, Manga, Ivumwe pamoja na Uwanja wa Sokoine. 


Lengo kuu la shughuli hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha Jiji la Mbeya linakuwa la kijani (Green City) kupitia uhifadhi wa mazingira na upandaji miti.


Akizungumza katika zoezi hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mbeya, Emmanuel Mwalupindi, amesisitiza umuhimu wa kupanda miti akieleza kuwa miti ina mchango mkubwa katika kulinda mazingira, kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha afya ya jamii.


Ameongeza kuwa upandaji miti unapaswa kuwa utamaduni endelevu kwa kila mwananchi ili kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinanufaika na mazingira bora na salama.






Post a Comment

Previous Post Next Post