
Na Mwandishi Wetu – Kilimanjaro
Mahakama ya Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, imewatia hatiani watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa makosa ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, na kuwaamuru kutumikia kifungo cha nje cha miezi 12 pamoja na kurejesha kiasi cha Sh milioni 12 walizotumia kinyume cha sheria.
Washtakiwa hao ni Mohamed Khalfan Bakari, aliyekuwa Mhasibu wa Mapato, na Laurent Abiud Mgonja, aliyekuwa Mkusanya Ushuru. Walipatikana na hatia ya makosa ya matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na kuisababishia Serikali hasara.
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, fedha hizo zilitokana na ukusanyaji wa ushuru wa mazao katika eneo la Makiwaru, ambapo walitakiwa kuziwasilisha kwenye akaunti ya Halmashauri lakini walizitumia kwa manufaa binafsi.
Shauri hilo lilisikilizwa na Hakimu Mkazi, Mhe. Elibahati Petro, huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Bi. Suzan Kimaro.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment