" MBEYA KUONJA LADHA YA MARATHON KABLA YA TUKIO KUBWA MEI

MBEYA KUONJA LADHA YA MARATHON KABLA YA TUKIO KUBWA MEI

Na Lydia Lugakila-Misalaba Media 

Mbeya 

Katika kuhamasisha mazoezi na kukuza michezo ndani ya jamii, Taasisi ya Tulia Trust kswa kushirikiana na Mbeya Jogging Club imeandaa mbio maalum zijulikana zo kama Pre-Betika Mbeya Tulia Marathon, zitakazofanyika Aprili 25, 2026 jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 23, 2026, Mratibu wa Michezo wa Taasisi hiyo, Lugano Mwangosi, amesema tukio hilo ni sehemu ya maandalizi ya mbio kubwa ya Betika Mbeya Tulia Marathon, ambayo mwaka huu inaadhimisha msimu wake wa kumi.

Amebainisha kuwa mbio hizo kuu zinatarajiwa kufanyika Mei 15 hadi 16 katika Uwanja wa Sokoine.

Mwangosi ameeleza kuwa lengo la mbio hizo za awali ni kumtambulisha mdhamini mkuu pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi, huku pia zikilenga kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi ya pamoja kila mwisho wa mwezi.

Amesema mbio hizo zitakuwa za taratibu, zikianzia katika maeneo ya Kabwe, Mafiati, Sangu, Sinde, Ujenzi na Iyunga (Lift Valley), na kuhitimishwa katika Uwanja wa Sokoine, ambapo kutafanyika michezo mbalimbali ya burudani.

Miongoni mwa michezo hiyo ni mbio za mita 100, kukimbia na gunia, kuruka kwa urefu (long jump), pamoja na mashindano ya kukimbia huku mshiriki akiwa amebeba yai kwenye kijiko.

Kwa upande wake, Mratibu wa mbio hizo, Lwiza John, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba michezo ya watoto imepewa kipaumbele ili kuibua vipaji vipya vya riadha vitakavyoweza kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Akitolea mfano mafanikio ya mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindano ya Boston Marathon, Lwiza amesema mafanikio hayo yanaonesha umuhimu wa kuendeleza vipaji tangu ngazi ya chini.

Naye Mwenyekiti wa Tulia Trust Mbeya Jogging Club, Gabriel Mwaisanila, amesema vilabu vya jogging vina utaratibu wa kuandaa mbio za pamoja kila mwisho wa mwezi, lakini mbio za April zina umuhimu wa kipekee kutokana na maandalizi ya marathon hiyo kubwa.

Hata hivyo  amehimiza wananchi wa Mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani, ikiwemo Mbalizi, kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo, akisisitiza kuwa mbali na kuboresha afya, tukio hilo pia linatoa fursa ya kushiriki michezo mbalimbali na kuimarisha mshikamano wa kijamii.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post