Leo, Aprili 21, 2026 – Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mhe. Sefu Hassan Dauda, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa ALAT Taifa, amekamilisha rasmi hatua ya kurejesha fomu baada ya kukamilisha mchakato wa ujazaji wa nyaraka za kugombea nafasi hiyo ya uongozi wa kitaifa.Hatua hiyo inafanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa ALAT Taifa unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili 2026 katika Jiji la Arusha, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, ambapo viongozi wa Serikali za Mitaa kutoka mikoa yote nchini wanatarajiwa kushiriki.Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Mhe. Dauda ameeleza kuwa amejitokeza katika kinyang’anyiro hicho kwa lengo la kuimarisha uongozi wa Serikali za Mitaa, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya halmashauri, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa na Serikali Kuu kwa maendeleo ya wananchi.Ameeleza kuwa ALAT ni jukwaa muhimu la kitaifa inayozikutanisha Mamlaka zote za Serikali za Mitaa Tanzania (Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa, na Majiji) ili kushirikiana, kutetea maslahi yao, na kuboresha huduma kwa wananchi, atahakikisha analeta uongozi wa matokeo unaozingatia maono, uwajibikaji na utekelezaji wa haraka wa miradi ya maendeleo.Aidha, Mhe. Dauda amewaomba wajumbe wote wa uchaguzi kutoka halmashauri, miji, majiji na mikoa mbalimbali nchini kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo, akisisitiza umuhimu wa kufanya maamuzi yatakayochagua viongozi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.Amesema kumchagua yeye kuwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa ni kuchagua kiongozi mwenye maono, uzoefu na vitendo, akihimiza kauli mbiu ya “Chagua Mabadiliko” kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika AICC Arusha.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment